EMF Worldwide | Spiral Sweep - Swahili
The Balancing Work logo - click for Home Page

EMF Balancing Technique, LatticeLogic, The Symbol, UCL Tai Ji, Yoga for The Lattice, Reflections, The Waves


Mkondo Mzunguko (Pia) wa Nguvu

Mwendo wa nguvu wa mzunguko (mfano wa Pia) ni zoezi ndogo lakini lenye umuhimu mkubwa katika ujumbe unapatikana katika mfumo wa mbinu ya kusawazisha mfumo huu wa EMF Balancing Technique®. Kupitia zoezi hili linatuwezesha kutayarisha mwili wa nguvu kwa nguvu thabiti tunazoweza kuwa nazo na kuzitumia katika maisha ya kila siku. Kama vile wengi wetu wanavyogundua, tukio la kitakatifu tulilokuwa tukitafuta limepatikana, yaani maisha yetu wenyewe. Zoezi hili linaweza kusomwa pole pole ukitaka, lakini unapolizoea, unaweza kwenda kasi uwezavyo. Unaweza kujionea jinsi nguvu zinavyoenea kitaswira jinsi unavyosoma kuanzia nambari moja hadi kumi na mbili.

1 - Kigezi Cha Kiunzi Cha Mifupa

Gusa, hisi, fikiri kuhusu nguvu muhimu zikizunguka nyayoni mwako kwa mzunguko wa mwondoko wa Akrabu. Ruhusu nguvu hizi zipenye nyayoni mwako. Mchanganyiko wa madini wa mifupa yake unafanya kiunzi chako cha mifupa kuwa njia mwafaka ya kupitishia nguvu zilizochujwa.

Sasa mfupa kwa mfupa, elekeza nguvu hizi muhimu kupitia kwa mfumo wa kiunzi cha mifupa. Elekeza nguvu hizo kupitia kwenye mifupa ya vidoleni mwako, mifupa yote katika nyayo, vifundo vya miguu hadi mwako magotini, vifuu vya magoti na kupitia mifupa katika mapaja. Elekeza nguvu hizo kupitia kwa mifupa ya nyonga kwenda chini hadi kifandugu/kitokono, kwenda juu hadi kwa uti wa mgongo. Osha kila pingili la uti wa mgongo na nguvu hizi muhimu. Elekeza nguvu hizo zitembee kupitia kwa hiyo mifupa kwenye mabega yako na mitulinga, kwenda chini hadi kwa mfupa wa kidari na kuzunguka mbavu zako. Zielekeze hizo nguvu muhimu kupitia kwa viganja vyako hadi na hata mifupa yote midogo midogo ya mkono na vidole. Sasa elekeza mawazo yako na nguvu juu hadi kwa shingo, tayani, kupitia kwa meno na fuvu zima.

Sasa umeosha kiunzi chako kizima cha mifupa yako na nguvu hizo muhimu. Sasa achia hisia zako, maoni yako/taswira ya kupenya huo mng'ao kote kwenye mifupa ya mwili mzima.

Vuta pumzi ndani halafu pumzika.

2 - Kigezi Cha Ubongo

Elekeza mawazo yako ndani ya ubongo wako mtakatifu na uiruhusu dhamira yako iingie ubongoni nguvu hizo. Anza kwa tabaka la nje la ubongo, hadi kwa maada ya girei ya ubongo, inayofunika sehemu ya ubongo ya juu. Chini ya sehemu hii, kunayo sehemu ya maada nyeupe, ambayo ndiyo sehemu kubwa zaidi ya ubongo. Iruhusu sehemu hio kuvuta nguvu hizo muhimu kama mfano wa sifongo. Uadilifu sharti usawazike na "hisi" ya nguvu hizo muhimu kupitia sehemu zote za ubongo. Mojawapo ya shughuli za maada hii nyeupe ni kusaidi utambuzi wa hisi za nguvu ziada.

Angazia mawazo yako baina ya nyusi juu zaidi hadi inchi moja hii ndani ya ubongo wako. Hapa utaweza onyesha ubongo, tezi ndogo yenye umbo la pojo. Elekeza nguvu hizo muhimu siweze kuzunguka kabisa hiyo tezi, na baadaye toa dhamira ili nguvu hizi zimezwe kabisa. Jinsi unavyopitisha nguvu hizo kupitia kwa hio tezi, toa dhamira ya kuamsha mabadiliko ya homoni katika mwili wako ambayo yatakuwa mwafaka zaidi kwako kwa kadri unavyofanya hatua ya mageuzo ifuatayo. Ubongo ndio ncha-chonge ya kwanza kabisa ya mguso inayounganishwa na tezipiniali.

Sasa weka mawazo yako katikati ya ubongo. Hii ndio sehemu ambayo wakati mwengine huitwa chemba kitakatifu. Hapa utapata tezipiniali. Ni tezi ndogo ya umbo la figo. Elekeza nguvu hizo kuzunguka tezi hii na baadaye ipe dhamira tezi hio imeze nguvu zote muhimu iwezavyo.

Pia utaona ya kwamba katika sehemu hii ya ubongo, kuna hipothalamasi na Thalamasi. Yako ni ogani yenye umbo la feni/pepeo yenye maada za girei zilizofungamanishwa na nyeupe. Sehemu hizi mbili za thalamasi zinapatikana katika nusu tufe zako mbili za ubongo.

Thalamasi ina wajibu wa nguvu za kuleta mawazo uliyonayo sasa hivi. Hebu chora taswira ya kipepeo muhimu sasa wakati ambao Thalamasi yako inaleta mwanga mzuri zaidi! Ipe dhamira yako uwezo wa kuongeza maelezo juu ya maumbile matakatifu.

Lete mawazo yako kichwani mwako sasa. Angalia ndani ya ubongo wako. Hapa unaona ogani yenye umbo mfano wa yai iitwayo poni. Fikiri kuhusu ogani hio kama limeangazwa na mwanga wa ajabu kabisa na kufunikwa. Hatimaye huku ukiwa na dhamira nzito elekeza nguvu mwelekea chini hadi kwa uti wako wa mgongo. Imeupatia ubongo wako nguvu za ajabu.

Vuta pumzi ndani na upumzike.

3 - Mfumo wa Endokraini

Regesha tena fikra zako na utaanza kuelekeza nguvu hizo muhimu zikishuka kupitia kwa mfumo wa endokraini.

Kwanza zingatia nguvu hizi muhimu zilizoko ndani ya Koromeo na tezi Koromeo katika sehemu ya chini ya koo. Iruhusu dhamira yako kumeza nguvu hizi za ajabu kabisa na kuziingiza kazi tezi hizo.

Juu ya moyo, chini ya kidevu, kuna tezi thamasi. Sehemu - nguvu muhimu inayohusiana na tezi hizi huitwa sehemu kati ya moyo ya juu. Tezi hii na nguvu za sehemu hii ni sehemu muhimu ya chanzo cha unusurishaji wa hiyo nguvu katika miili yetu. Kuzidi kwa usambazaji huu wa nguvu kutoka kwa juu ya moyo ni mojawapo ya ufunguo kwa maelezo dhabithi ya maumbile yetu ya kiroho-umeme. Jinsi tunavyoongeza uwezo wetu wa kuieleza hii nguvu-umeme, tunaweza kuongeza njia ya uponyaji wakati mwili haukusawazika. Ni maazimio yetu ya kuamsha sehemu hii ya mwili. Elekeza nguvu hizi kuzunguka kwa thamasi yako na kuimeza yote kabisa. Sizitisha nia zako huku tezi thamasi ikijaa na mng'ao. Nitafikia kiwango cha kujitosheleza halafu nisambaze nguvu hizo kote kwenye chembechembe za moyo mzima. Pigia taswira moyo wako wote jinsi unavyosambaza mng'ao huo!

Elekeza mawazo yako katika misuli ya moyo. Moyo si sehemu ya mfumo wa endokrain. Hata hivyo utando wa moyo kifuko kinachofunika moyo kinaweza kujazwa na matone ya thamani ya ugiligili wa homoni. Ugiligili huu utachangia mwongezeko wa usambazaji wa nguvu za moyo. Ipe dhamira yako iweze kujaza moyo wako na nguvu hizo za mageuko na upendo.

Upande wa kushoto wa kitovu ni wengu na tunapojaribu kuamsha ogani hii kwa kutumia nguvu hizo, ipe dhamira ili iongeze uwezo wako wa kuendelea kusaga na kulishiza mabadiliko haya na nguvu yanayofanyika katika mwili mzima.

Sasa egesha mawazo yako katika sehemu ya nguvu ya tezi ya adrenalini. Adrenalini hii hukaa juu ya figo. Tumia mwangaza huu na uupe dhamira ili uwezo wa kuongoa tena tezo za adrenalini.

Chini kidogo lete mawazo kwenye tezo za ujinsia, ovari na makende halafu uzuie nguvu hizo ndani ya sehemu hii ya mwili wako. Mchangamsho huu ni kwa kila chembechembe ya mwili wako hata chembechembe zilizo chini ya kiuno chako.

Elekeza nguvu zako chini hadi kwa nyonga, mapaja, viwiko na nyayo za miguu yako. Mwili mzima umeingizwa nguvu kufikia hapo.

Pumua kwa nguvu kasha pumzika.

4 - Nguvu Zilizoko Miguuni

Nguvu hizi sasa zinazunguka kwenye miguu yako na kuleta athari nzito. Kwa kufahamu umuhimu wa kuwa na uhusiano mzito wa nguvu za dunia. Udhibiti huu mtakatifu huchangia katika uwezo wetu wa kuweza kuhimili nguvu nyingi zaidi tulizonazo.

Marudio ya mitetemeko ya nguvu hubadilisha nakuleta mwinuko wa polepole katika baka la nguvu kama miale ya mwanga iliyokusanyika pamoja na nguvu. Tutaelekeza miale hii ya mwanga kupitia kwa mizingira ya nguvu hizo ambayo inahusishwa na mifumo ya tezi.

Mabadiliko ya nguvu wakati mwingine hutambulika kama mabadiliko ya joto au hizi za mchonyoto kadri unavyoelekeza nguvu kupitia kwa vizinga vya nguvu kwenye miguu, kupitia kwa nguvu za miguu mpaka kwa chini ya mtulinga.

5 - Sehemu Muhimu

Elekeza mawazo yako chini ya mtulinga na uhisi, uguse, ufikiri na kuwaza juu ya tufe ling'aalo kwa rangi nyekundu, nguvu muhimu. Jinsi miale hii inavyopenya kwenye tufe hilo, ruwaza ipendezayo mfano wa nyota iliyopasuka huanza kujiunda na kusambaa pande zote. Ipe dhamira uwezo wa kubariki, kuthibiti na kusawazisha nguvu katika sehemu ya chini ya mtulinga wako. Kadri unavyofanya hivyo, unajenga msingi wa kitakatifu katika ubinadamu wako unaohujika kadri unavyoendelea kuchanganya nguvu za maumbile yako matakatifu.

Miale hiyo ya mwanga hupanda hadi eneo jipya la nguvu katika uumbaji/eneo la ujinsia.

6 - Uumbaji/Eneo La Uzazi

Kadri miale ya nguvu inavyopaa kuelekea eneo la ujinsia, elekeza mawazo yako katika tufe la rangi ya machungwa la uumbaji. Mwangaza huu husambaa katika kwenye tufe hili la rangi ya machungwa lote kila mara katika ruwaza ya nyota iliyopasuka. Ipe dhamira yako uwezo wa kufikiria jinsi unavyoeleza nguvu za uzazi. Nguvu zako za uzazi ni sehemu ya msukumo muhimu wa uhai na unaweza kuelekezwa ili kuwezesha mageuko yako. Sehemu hii pia ni makao ya uumbaji. Ziwezeshe nguvu hizo zisambae kutoka sehemu hii ili ilete uwezo wa uhuluku wako wa maisha. Ipe dhamira yako uwezo wa kubariki, thibiti na sawazisha eneo hili la uzazi.

Vuta pumzi.

7 - Eneo la Mishipa ya Fahamu (Nyuma ya tumbo)

Sasa miale hiyo ya nguvu inapanda juu. Elekeza nguvu hizo kuingia katika tufe la manjano katika mishipa ya fahamu. Kadri nguvu hizi zinavyotoa mwangwi ndani ya eneo hili, unaweza kugusa, kuhisi, kufikiri na kuwaza juu ya ruwaza zinazoonekana kama halizeti.

Kumbuka kwamba mishipa hii ya fahamu pia huitwa makao ya akili iliyofichika na vipengere vyote vya mfano wa halizeti inayong'aa yatu kumbusha vipengere vyote tulivyonavyo.

Vuta pumzi nyingi na jiruhusu kuwa!

8 - Eneo la Moyo wa Eneno la Juu la Moyo

Sasa elekeza mawazo yako na miale ya nguvu juu zaidi katika zumaridi zuri la kijani kibichi ndani ya moyo wako.

Hisi-nguvu hizo zikipasuka katika nelibini inayopendeza ya nguvu hizo za kijani ikidunda katika ruwaza tata. Kila mmoja wetu amebeba kipande asili cha Muumba katika moyo wetu, na pamoja tunaomba.

Elekeza mawazo yako juu ya moyo kwenye sehemu iitwayo thamasi, sehemu hii huitwa sehemu ya juu ya eneo la moyo. Hapa utapata mkusanyiko wa miale. Ipe dhamira yako uwezo kuongeza mwangaza huo. Utahisi joto na ukamilifu wa moyo wako kadri ambavyo ruwaza ya mwangaza wa kipekee wa nguvu za moyo wako ikijifungua. Unavyohisi usawa ndani ya moyo wako, kuza ubinafsi wako, kwa upendo na usambaze upendo huo nje yako.

9 - Eneo La Roromeo

Kadri nguvu ya upendo zinavyoendelea kusambaa nje, elekeza miale hiyo juu na hadi ndani ya rangi ya samawati ndani ya Roromeo lako. Eneo hili ni njia muhimu; ndio sehemu ambayo nguvu zinaungana (sio juu wala chini), na hugeuzwa nguvu-tumika. Hili ndili eneo la kueleza ukweli wako. Kumbuka nguvu neno lililotamkwa. Jizatiti uzungumze ukweli pekee, hata kama ni kwa uchache zaidi. Ruhusu nguvu zikusawazishie njia ya kujieleza ulimwenguni.

Unaweza geuza kichwa chako polepole kutoka upande mmoja hadi mwengine kadri unavyoisukuma nguvu hiyo kupitia kwa eneo la koo. Uko karibu kumaliza zoezi hili.

Pumua kwa nguvu na chunguza tena mawazo yako.

10 - Jicho La Tatu

Sasa kusanya pamoja na elekeza miale yako ya nguvu juu kupitia kwa sehemu ya kati ya ubongo wako. Kutoka kwa sehemu ya kati ya ubongo hadi kwa tezi ubongo karibu na sehemu ya kati ya kipaji ndiyo sehemu tunayoiita jicho la tatu. Hapa nguvu hugeuka na kuwa rangi ya nili. Kadri miali inavyosambaa taratibu kupitia kwa sehemu ya kati ya rangi ya nili, ruwaza za mwanga hufanana na vipengee mchanganyiko vya taya. Ipe dhamira yako uwezo wa kuingia ndani ya hekima ili upate uwezo zaidi wa kuelewa mambo. Unaweza kujiwazia maana ya "fikiri kwa moyo wako na hisi kwa akili yako". Sehemu hii pia inahusishwa na uwezo wa kupashana mawazo bila ya kutumia njia za hisia za kawaida-Hisi ya sita tunayoiunda kwa haraka sana hivi sasa.

11 - Eneo la Utosi

Regelea kuangaza na kuongeza mawazo yako kadri unavyoelekeza mwanga huo kupitia kwa eneo la utosi. Kadri nguvu hizi zinavyozunguka kwa ushwari juu ya kichwa chako, ruwaza ya kipekee ya mwanga, mzunguko hujiunda. Hii ni ruwaza ya nguvu ya ushirika. Nguvu zako za maumbile ya kibinadamu huungana na uzuri wa maumbile ya kitukufu.

12 - Zuia na Uachilie

Sasa pumua kwa undani kupitia kwa pua yako na ukwamize hewa hiyo kwa muda, wacha nguvu zijiunde. Kwa dhamira nzito, toa pumzi, kupitia kwa mdomo, kadri unavyofanya hivyo, chora taswira ya mchipuo wa nguvu za kila rangi zikipaa juu hadi kwa kichwa chako na baadaye zikizunguka hadi chini kupitia na kuenea mwili mzima. Mwenendo huu unathibiti viunzi vyako na kustawisha muungano wako na nguvu za dunia. Burudika kwa muda mfupi. Utahisi hisia za kuwa huru.

Namaste, rafiki mpendwa.

Hii ndio tamati ya zoezi hili.